Skip to main content

VYAKULA WAKATI WA UJAUZITO

FAHAMU VYAKULA VINAVYOFAA NA VILE VINAVYOZUILIWA WAKATI WA UJAUZITO Dr. DALUS
Ni vyakula gani vya kuepuka kutumiwa na wajawazito? Ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili timamu, akiwa tumboni lazima alishwe lishe bora na mlo sahihi.
Mwenye jukumu la kutoa lishe bora na sahihi kwa kiumbe kilichomo tumboni ni mama. Anatakiwa kujua aina ya vyakula anavyopaswa kula. Vivyo hivyo, anatakiwa kujua aina ya vyakula vya kuviepuka.

Katika makala ya leo, tunaangalia orodha ya vyakula vilivyokatazwa. Mama mja mzito haruhusiwi kuvila vyakula vifuatavyo kwa faida ya kiumbe kilichomo tumboni na kwa faida yake mwenyewe:

Nyama mbichi Epuka kula samaki au nyama mbichi au iliyopikwa lakini haikuiva vizuri.
Utajiepusha na uwezekano wa kula bakteria na vijidudu vingine hatari kwa afya ya mtoto tumboni.
Mjamzito anapokula nyama, anatakiwa kuhakikisha imeiva sawasawa. ‘Soseji” na “Sandwich” Mjamzito haruhusiwi kula ‘soseji’, ‘sandwichi’ za nyama na vyakula vingine vilivyotengenezwa kwa nyama. Inaaminika kuwa nyama zinazoandaliwa kwa ajili ya kutengenezea vyakula kama hivyo, huwa vimewekewa vihifadhi vyakula (preservatives) ambavyo vinaweza visiwe vizuri kwa afya ya mtoto.

Samaki wenye zebaki (Mercury) Wajawazito wamekatazwa kula samaki wenye kiasi kingi cha madini ya zebaki. Ulaji wa zebaji kwa wajawazito umehusishwa na uzaaji wa watoto taahira.
Mfano wa samaki hao ni pamoja na Papa, Chuchunge na dagaa wakubwa. Mayai Mabichi Ulaji wa mayai mabichi au vyakula vilivyochanganywa na mayai mabichi, mjamzito haruhusiwi kuvila. Kuna baadhi ya ‘Ice Cream’ na ‘mayonaizi’ hutengenezwa kwa kuchanganywa na mayai mabichi.
Mjamzito amekatazwa kuvila vyakula hivyo. Maini Maini yana kiwango kikubwa cha madini aina ya chuma. Hata hivyo, yana kiasi kikubwa cha Vitamin A ambacho huweza kuwa na madhara kwa mtoto kikizidi.
Maziwa mabichi Maziwa mabichi huweza kuwa na bakteria ajulikanae kama ‘Listeria’, ambaye huweza kusababisha kuharibika kwa mimba.
Unapokunywa maziwa, hakikisha yamechemshwa au kama ni ya paketi hakikisha ni yale yaliyoandikwa‘Pasteurized’ na siyo ‘Unpasteurized’.

Kafeini (Caffeine) Ingawa baadhi ya utafiti unaonesha kuwa unywaji wa kiasi kidogo cha kafeini hauna madhara, lakini kuna utafiti mwingine unaonesha kuwa unywaji wa kafeini una uhusiano na kuharibika kwa mimba.
Kafeini ni aina ya kirutubisho kinachopatikana ndani ya kahawa. Iwapo mjamzito atakunywa kahawa, basi anywe kiasi kidogo sana kisichozidi kikombe kimoja kwa siku.
Kwa kawaida kahawa hukausha maji mwilini, hivyo unywaji wake husaidia kukauka maji mwilini ambayo ni muhimu sana kwa mjamzito.
Utafiti mwingine unaonesha kuwa kafeini inahusishwa pia na uharibikaji wa mimba, uzaaji wa watoto ‘njiti’ na watoto wenye uzito mdogo.
Ni vizuri kunywa maji ya kutosha, maziwa na juisi na kuepuka kunywa vinywaji vyenye kahawa.

Unywaji wa pombe wakati wa ujauzito huweza kuathiri ukuaji mzuri wa mtoto. Kutegemeana na kiasi atakachokunywa mjamzito, pombe inaweza kumsababishia mtoto ugonjwa hatari utokanao na pombe (Fetal Alcohol Syndrome).
Vyakula gani ni muhimu sana kutumiwa na wajawazito? Lishe bora wakati wa ujauzito ni muhimu sana, kwani lishe hii hutumika kwa mama na mtoto anaendelea kukua tumboni.

Kwa kawaida mahitaji ya chakula na virutubisho mwilini mwa mwanamke huongezeka wakati wa ujauzito na kadri ujauzito unavyoendelea kukua, virutubisho hivyo hutumika kujenga mwili wa mama na mtoto.

Hivyo maamuzi ya lishe au lishe mama anayopata huathiri pia maendeleo ya mtoto anayekua mwilini mwake. tutaona vyakula muhimu vya kuzingatia lishe bora wakati wa ujauzito na baadhi ya vitu vya kukwepa.

Mlo kamili (balanced diet), ni muhimu kwa ajili ya maendeleo mazuri ya afya ya mjamzito na mtoto tumboni.
Pamoja na mlo kamili mjamzito hupewa virutubisho ziada (supplements) kwa ajili ya kuongeza madini kama ya chuma na Foliki.

Mlo kamili unajumuisha vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini:
Nafaka na vyakula vya wanga Vyakula hivi huupa mwili nguvu za kufanya kazi ikiwemo ukuaji wa mtoto tumboni. Vyanzo vya wanga ni kama nafaka mbalimbali(mahindi,mtama,ulezi n.k), viazi, ndizi, mihogo.

Ni vizuri mjamzito awe anapata nafaka kamili(whole grains) kama mahindi, ngano na mchele usiokobolewa; cereals n.k.

Nyama, samaki na vyakula vya protini Hivi ni muhimu kwenye kuujenga mwili, hasa kipindi cha miwezi wa 4 mpaka wa 9 ambacho viungo mbalimbali vya mtoto vinajengwa.
Ni muhimu mama apate vyakula vya protini vya kutosha ili kuhakikisha ukuaji wa mtoto unaenda vizuri.
Nyama za kuku, ng’ombe, mbuzi, senene, panzi na wanyama wengine ; vyanzo vya protini za mimea kama maharage, soya, njugu, njegere, karanga,korosho n.k . Samaki, maziwa, mayai ni vyanzo vingine vya protini muhimu .

Vyakula vya mafuta Hutumika kwenye kuupatia mwili nguvu pamoja na ujengaji wa seli za mwili.
Mara nyingi vyakula kama nyama, karanga, ufuta, alizeti,senene, panzi, samaki na matunnda kama maparachichi huwa na mafuta.
Ni vizuri kutumia mafuta yatokanayo na mimea ili kupunguza mafuta yenye lehemu(cholesterol) nyingi.

Mboga za majani na matunda Matunda na mboga za majani ni sehemu muhimu sana ya mlo wakati wa ujauzito, kwani huupatia mwili vitamini, madini na kambakamba kwa ajili ya kulainisha chakula.
Vitamini husaidia kuimarisha kinga ya mwili sambamba na ufanyaji kazi wa mwili.
Madini kama ya chuma, kalsiamu, zinki, madini joto(Iodine) na magneziamu ni muhimu kwa ukuaji salama wa mtoto tumboni mwa mama.
Vitamini B9 (Foliki asidi) na madini ya chuma hutolewa kama virutubisho ziada kliniki wakati wa ujauzito ili kutosheleza mahitaji ya mwili na kuzuia hatari ya upungufu wa damu kutokea.

Maji Maji ni muhimu kwenye mmenyenyo na unyonywaji wa chakula, pia husaidia kuzuia choo kigumu, mwili kuvimba na maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI). Inashauriwa mjamzito anywe maji si chini ya lita 2.3 kwa siku, yanaweza kuwa katika chai, juisi, soda, au maji yenyewe.

Ni vema zaidi kama akinywa maji kama maji zaidi na kupunguza vinywaji kama soda.
Mfano wa mpangilio wa mlo Ili kuhakikisha mlo kamili mjamzito anaweza kufuata mfano wa mpangilio wa mlo ufuatao.
Katika mpangilio huu inashauriwa kuchagua aina moja ya chakula kutoka katika kila herufi A mpaka E ili kuweza kuupata mlo kamili. Mfano:
Mlo wa Asubuhi:
A – Chungwa/ Embe/ Ndizi mbivu/ Parachichi
B – Mkate/ Maandazi/ Chapati/ Vitumbua/ Uji C – Karoti
D – Mayai
E – Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya Soya

Mlo wa Mchana:
A – Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na chungwa
B – Ugali/ Wali/ Ndizi/ Makande/ Tambi
C – Mchicha/ matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji
D – Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa
E – Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya Soya.

Mlo wa Usiku:
A – Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na Chungwa
B – Wali/ Ndizi/ Viazi/ Tambi/ Chapati
C – Mchicha/ Matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji,
D – Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa
E – Maziwa/Mtindi/Siagi/Maziwa ya Soya.

Comments

Popular posts from this blog

BIMA YA AFYA NA FAIDA ZAKE

BIMA YA AFYA NA FAIDA ZAKE By Dalus Bima ya afya ni nini? Bima ya afya ni mfumo wa kujiunga kwa hiari ama kwa lazima unaomhakikishia mwanachama kugharamiwa gharama zozote zinazojitokeza katika kupata huduma za kiafya zikiwemo kumwona daktari, kufanya vipimo pamoja na kupata matibabu na dawa kwa mwanachama husika. Bima ya afya ni kama mkataba unaoingiwa na anayetaka huduma pamoja na mtoa huduma kwa kupitia mifuko au taasisi inayowaunganisha mtoa huduma pamoja na mhitaji wa huduma husika. Mara nyingi Bima ya afya hujumuishwa kwenye makato anayoyatoa mwajiri kwa waajiriwa wake katika kufanya malipo. Pia zipo bima zinazowahusu watu binafsi, wazee na wasiojiweza, wajawazito na wengine wenye mahitaji maalumu bila kusahau wanafunzi kipindi cha masomo yao. Mara nyingi wanachama huchagua taasisi ama mifuko inayotoa bima hizi kulingana na aina, viwango na mipaka (coverage) ya Taasisi/Bima hizo. Ni ukweli uliowazi kuwa kila mfuko huweza kutofautiana na mingine katika huduma inazozitoa kwa...

FAIDA ZA NDIZI MWILINI

FAIDA ZA NDIZI MWILINI Ndizi mbivu ni tunda linalotumika sana kama mlo sehemu mbalimbali duniani. Ni tunda ambalo ni tamu na lenye virutubisho mbalimbali na muhimu kwa mwili. Baadhi ya faida za ndizi kiafya ni kusaidia moyo kufanya kazi vizuri, kupunguza uwezekano wa kupata saratani na pumu. Ndizi ni chanzo kizuri cha madini ya Potasiamu. VIRUTUBISHO VILIVYOMO KWENYE NDIZI Ndizi ya wastani ina uzito wa kama gramu 126O. Ina nishati kiasi cha kalori 110, gramu 30 za wanga na gramu 1 ya protini. Ndizi hazina fati, lehemu (cholesterol) au madini ya Sodiamu. Ndizi zina virutubisho  vifuatavyo; Vitamini B6 – 0.5 mg Manganizi- 0.3 mg Vitamini C – 9 mg Potasiamu – 450 mg Kambakamba- 3g Protini – 1 g Magneziamu – 34 mg Madini ya Foliki- 25.0 mcg Riboflavin – 0.1 mg Niacin – 0.8 mg Vitamini A – 81 IU Madini ya chuma – 0.3 mg FAIDA ZA NDIZI KIAFYA Kushusha Shinikizo la Damu Ndizi zina madini ya Potasiamu kwa wingi amb...

MTOTO KATIKA UKUAJI

HATUA MUHIMU ZA UKUAJI WA MTOTO KISAIKOLOJIA Dr. DALUS Mtoto anapitia mabadiliko mbali mbali ya kimwili,kiakili na kisaikolojia pindi anapokua anakuwa hadi kuwa mtu mzima. leo nitakuelezea hatua za ukuaji wa mtoto kisaikolojia muhimu sana katika malezi yake. hatua hizo ni kama ifatavyo 1.ORAL STAGE Mtoto anakua katika stage hii anapokuwa na umri wa,mwezi mmoja hadi mwaka mmoja.   Sasa kwa kipindi hiki erogenous zone ya mtoto inakua mdomoni, raha ya mtoto inakua kitu chochote kinachoingia mdomoni ndo maaana kipindi hiki mtoto kila kitu anachoshika anapeleka mdomoni . Hiki ndo kipindi cha kujenga strong bond kwa mtoto na mama pale mtoto anapokuwa ananyonya inamjenga kumthamini mama kuliko mtu yyte Kipindi hiki inabdi kuwa makini na vitu kama shanga,sarafu nk ambavyo akiweka mdomoni vnaweza kumkaba Hapa kama mzazi ana tabia ya kula kucha ndo kipindi mtoto nae anajifunza na kua hvo anapokua 2.ANAL STAGE Stage hii inaanza umri wa mwaka 1 hadi miaka mi 3 Hapa mtoto raha yake ni ...