Skip to main content

FISTULA

FAHAMU ZAIDI KUHUSU FISTULA
By Dr. DALUS
Kwa kitaalamu fistula hujulikana kama njia isiyo ya kawaida inayounganisha mfuko wa mkojo na uke, ambayo huruhusu mkojo na/au haja kubwa kutoka  bila kujizuia kwenye kuta za uke. Nini hutokea?

Tatizo la kushindwa kujizuia kujikojolea na/au kupitisha haja kubwa kwenye tupu ya mwanamke linalojulikana kama fistula hutokea baada ya mwanamke kupata madhara kipindi cha kujifungua kutokana na kuwa kwenye uchungu wa kujifungua kwa muda mrefu (Prolonged and obstructed labor), kutokana na kichwa cha mtoto kushindwa kupita kwa urahisi kwenye tupu ya  mwanamke.

Hali hii husababisha tishu za kwenye tupu ya mwanamke, kibofu cha mkojo na puru (rectum), kugandamizwa kati ya kichwa cha mtoto na nyonga za mwanamke.

Hii husababisha mfumo wa damu kwenye tishu hizi kuharibika na tishu kukosa damu na kuwa katika hali inayojulikana kitaalamu kama ischemic necrosis.

Baadaye tundu hutokea kati ya tupu ya mwanamke na kibofu cha mkojo au kati ya tupu ya mwanamke na puru.
Matokeo yake ni mwanamke kutoa mkojo na/au haja kubwa bila kujizuia kupitia tupu yake (vagina).

Ukubwa wa tatizo Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linakadiria kuwa wasichana na wanawake wapatao millioni 4 duniani wanaishi na tatizo hili wakati kila mwaka wasichana na wanawake wengine 50,000 - 100,000 hupatwa na tatizo hili.

Fistula huonekana sana kwenye bara la Afrika na Asia ya kusini.
Kwa Tanzania, wanawake na wasichana 1,200 kila mwaka hupatwa na tatizo hili. Katika tafiti mbili zilizofanyika Tanzania, iliripotiwa kuwa wanawake walio katika umri kati ya miaka 22-24 ndiyo hupatwa na tatizo hili zaidi.

VVF husababishwa na nini? Uchungu wa muda mrefu (Prolonged labour) ambao husababishwa na Kutokuwa na usawa wa uwiano wa nyonga ya mama na ukubwa wa mtoto (CPD)

Mtoto kulala vibaya (malpresentation) Upasuaji wa kuondoa kizazi (hysterectomy)
Upasuaji wa njia ya mkojo (repair of urethral diverticulum, electrocautery of bladder papilloma) Upasuaji wa kansa za nyonga (pelvic carcinomas).

Dalili Mkojo kutoka  bila kujizuia kwenye kuba ya uke ndio dalili muhimu
Kuna uwezekano wa kupata maambukizi hivyo dalili zifuatazo huweza kuambatana na dalili ya mwanzo homa na maumivu ya tumbo hasa ubavu na chini ya kitovu.

Vipimo Majimaji yanatoka kwenye kuta za uke huchunguzwa vitu vifuatavyo: Urea, creatinine, na potassium ili kuwa na uhakika kuwa ni VVF na sio Vaginitis (maambukizi ya uke)
Mkojo huoteshwa kuangalia kama kuna vimelea na kujua dawa gani yaweza kuvimaliza vimelea hivyo

Rangi ya indigo carmine hutolewa kwa njia ya mshipa na pindi inapoonekana ukeni huthibitisha VVF Cystourethroscopy Intravenous urogram .

Matibabu Kama tatizo limegundulika siku chache baada ya upasuaji mpira wa kukojolea (urinary catheter either transurethral or suprapubic) huwekwa kwa siku 30.

Fistula ndogo (chini ya sentimita 1) huweza kupona yenyewe au kupungua. Upasuaji ili kurekebisha VVF, aina za upasuaji .

Vaginal approach Abdominal approach Electrocautery Fibrin glue Endoscopic closure using fibrin glue with or without adding bovine collagen Laparascopic approach Using interposition flaps or grafts .

Baada ya upasuaji Mgonjwa huwekewa Suprapubic catheter (mpira wa mkojo) kwa siku 6 hadi 60 ili kupunguza mvutano wa nyuzi .
Vitamin C 500mg mara tatu kwa siku ili mkojo uwe wa asidi ili kuzuia maambukizi na kutengenezwa kwa mawe.

Tiba ya kichochezi cha ostrogeni kwa wakina mama walikwisha acha kupata siku zao (postmenopausal) .
Dawa za kuzuia mshtuko wa mfuko wa mkojo-methylene blue na Atropine sulfate Antibaotiki .
Pumzisha nyonga kwa kuzuia tendo la ndoa kwa kipindi cha wiki 4 hadi 6. Ingawa wengine hushauri hadi miezi mitatu.

Comments

Popular posts from this blog

BIMA YA AFYA NA FAIDA ZAKE

BIMA YA AFYA NA FAIDA ZAKE By Dalus Bima ya afya ni nini? Bima ya afya ni mfumo wa kujiunga kwa hiari ama kwa lazima unaomhakikishia mwanachama kugharamiwa gharama zozote zinazojitokeza katika kupata huduma za kiafya zikiwemo kumwona daktari, kufanya vipimo pamoja na kupata matibabu na dawa kwa mwanachama husika. Bima ya afya ni kama mkataba unaoingiwa na anayetaka huduma pamoja na mtoa huduma kwa kupitia mifuko au taasisi inayowaunganisha mtoa huduma pamoja na mhitaji wa huduma husika. Mara nyingi Bima ya afya hujumuishwa kwenye makato anayoyatoa mwajiri kwa waajiriwa wake katika kufanya malipo. Pia zipo bima zinazowahusu watu binafsi, wazee na wasiojiweza, wajawazito na wengine wenye mahitaji maalumu bila kusahau wanafunzi kipindi cha masomo yao. Mara nyingi wanachama huchagua taasisi ama mifuko inayotoa bima hizi kulingana na aina, viwango na mipaka (coverage) ya Taasisi/Bima hizo. Ni ukweli uliowazi kuwa kila mfuko huweza kutofautiana na mingine katika huduma inazozitoa kwa...

FAIDA ZA NDIZI MWILINI

FAIDA ZA NDIZI MWILINI Ndizi mbivu ni tunda linalotumika sana kama mlo sehemu mbalimbali duniani. Ni tunda ambalo ni tamu na lenye virutubisho mbalimbali na muhimu kwa mwili. Baadhi ya faida za ndizi kiafya ni kusaidia moyo kufanya kazi vizuri, kupunguza uwezekano wa kupata saratani na pumu. Ndizi ni chanzo kizuri cha madini ya Potasiamu. VIRUTUBISHO VILIVYOMO KWENYE NDIZI Ndizi ya wastani ina uzito wa kama gramu 126O. Ina nishati kiasi cha kalori 110, gramu 30 za wanga na gramu 1 ya protini. Ndizi hazina fati, lehemu (cholesterol) au madini ya Sodiamu. Ndizi zina virutubisho  vifuatavyo; Vitamini B6 – 0.5 mg Manganizi- 0.3 mg Vitamini C – 9 mg Potasiamu – 450 mg Kambakamba- 3g Protini – 1 g Magneziamu – 34 mg Madini ya Foliki- 25.0 mcg Riboflavin – 0.1 mg Niacin – 0.8 mg Vitamini A – 81 IU Madini ya chuma – 0.3 mg FAIDA ZA NDIZI KIAFYA Kushusha Shinikizo la Damu Ndizi zina madini ya Potasiamu kwa wingi amb...

MTOTO KATIKA UKUAJI

HATUA MUHIMU ZA UKUAJI WA MTOTO KISAIKOLOJIA Dr. DALUS Mtoto anapitia mabadiliko mbali mbali ya kimwili,kiakili na kisaikolojia pindi anapokua anakuwa hadi kuwa mtu mzima. leo nitakuelezea hatua za ukuaji wa mtoto kisaikolojia muhimu sana katika malezi yake. hatua hizo ni kama ifatavyo 1.ORAL STAGE Mtoto anakua katika stage hii anapokuwa na umri wa,mwezi mmoja hadi mwaka mmoja.   Sasa kwa kipindi hiki erogenous zone ya mtoto inakua mdomoni, raha ya mtoto inakua kitu chochote kinachoingia mdomoni ndo maaana kipindi hiki mtoto kila kitu anachoshika anapeleka mdomoni . Hiki ndo kipindi cha kujenga strong bond kwa mtoto na mama pale mtoto anapokuwa ananyonya inamjenga kumthamini mama kuliko mtu yyte Kipindi hiki inabdi kuwa makini na vitu kama shanga,sarafu nk ambavyo akiweka mdomoni vnaweza kumkaba Hapa kama mzazi ana tabia ya kula kucha ndo kipindi mtoto nae anajifunza na kua hvo anapokua 2.ANAL STAGE Stage hii inaanza umri wa mwaka 1 hadi miaka mi 3 Hapa mtoto raha yake ni ...