Skip to main content

MADHARA YA UNYWAJI YA POMBE WAKATI WA UJAUZITO

Madhara ya Unywaji wa Pombe wakati wa Ujauzito.
By Dr. DALUS

Kati ya mambo ambayo watu wengi hawatilii maanani sana ni unywaji wa pombe wakati wa ujauzito.
Nimekuwa nikiwaona akina mama wajawazito wengi wakinywa pombe kwenye sehemu za starehe na sherehe mbalimbali.

Hata hivyo si nia ya makala hii kuwazuia kunywa pombe bali kuwapa elimu sahihi juu ya unywaji wa pombe wakati wa ujauzito.
Baadhi ya wataalam wanasema unywaji wa wastani wakati wa ujauzito ni kitu ambacho kinaweza kukubalika ingawa wapo baadhi ya wataalamu wengine wanaoamini kuwa unywaji wa hata glasi moja ya mvinyo (wine) kwa wiki huhatarisha afya ya mtoto wako.

Hata hivyo haijulikani kwa hakika, ni kiasi gani cha pombe ni salama kwa makuzi sahihi ya mtoto wako tumboni. Wataalamu wengi wanashauri kuacha pombe kabisa wakati wa ujauzito.

Pombe inaweza kuleta madhara makubwa kwa mtoto wako bila wewe kuhisi madhara yake.
Na yanaweza kuwa madhara ya kudumu ambayo ataishi nayo maisha yake yote.

Aidha kuna dhana imejengeka kwa baadhi ya wajawazito kuwa, hawatakiwi kunywa pombe kali kama vodka au whisky tu lakini ni ruksa kutumia aina nyingine za pombe.
Hata hivyo dhana hii si sahihi kwa kuwa pombe za aina zote zaweza kuleta madhara makubwa kwa kiumbe aliye tumboni.
Kisayansi takwimu zinaonyesha kwamba unywaji sana wa pombe wakati wa ujauzito huathiri mimba.
Ni hili hutokea zaidi katika kipindi cha miezi 3 ya mwanzo (first trimester), kipindi ambacho viungo vingi vya mwili wa mtoto hufanyika (organogenesis).

Nini hutokea unapokunywa pombe wakati wa Ujauzito?
Pombe ni sumu kwa mtoto. Unapokunywa pombe inaingia moja kwa moja kwenye mzunguko wa damu wa mama kasha hufika kwa mtoto kwa kupitia kondo la nyuma (placenta).

Mara pombe inapoingia kwenye mzunguko wa damu wa mtoto, huathiri uwezo wa mtoto kupata chakula, virutubisho na oksijeni ya kutosha kwa ajili ya maendeleo ya kawaida katika ubongo na viungo vingine.
Hii inaweza kuathiri ubongo wa mtoto na ukuwaji wa viungo vya mwili kwa ujumla. Uharibifu huu unaweza kuathiri uwezo wa mtoto kujifunza na kufikiri pindi anapozaliwa hali ambayo itajionesha kwa matendo yake kama mtoto na kama mtu mzima.

Aidha, utafiti umeonesha kwamba uwezo wa mimba kustahimili kiwango cha pombe ni mdogo mno hali ambayop huathiri ufanyikaji wa viungo na ukuwaji wake kwa kiasi kikubwa.

Kwa kiasi gani mtoto wako ambaye hajazaliwa anaweza kuathiriwa na pombe?
Kiwango cha kuathirika kwa mimba kutokana na unywaji pombe unaofanywa na mama mjamzito hutegemea sana mambo makuu matatu ambayo ni:
Kiasi cha unywaji wa pombe hatua ya mimba yaani umri wa mimba mara ngapi unakunywa pombe Matatizo yatokanayo na unywaji wa pombe
Baadhi ya madhara yanayoweza kumpata kiumbe aliye tumboni kwa mama kutokana na unywaji wa pombe kipindi cha ujauzito ni pamoja na

Kutoka/kuharibika kwa mimba
Mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo Mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu wa mbavu na kidari (sternum)
Mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya mgongo uliopinda (kibiongo) na vidole vilivyoundana
Mtoto kuzaliwa akiwa na kichwa kidogo kuliko kawaida (microcephaly)
Mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya pua Kuzaliwa na matatizo ya taya
Mtoto kuwa na matatizo ya kutokuona mbali Matatizo ya moyo kama vile moyo kuwa na tundu Matatizo ya figo
Mtoto kuwa na ubongo mdogo na pia matatizo ya akili
Mtoto kuzaliwa akiwa na mdomo sungura (lip palate na cleft palate)
Matatizo ya kimaumbile ya masikio na ulemavu kwenye sehemu za uzazi (genital malformations).

Aina mojawapo ya kansa ya chembe nyeupe za damu (Acute Myeloid Leukemia).
Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida moja la utafiti wa kansa la Marekani lijulikanalo kama Journal of the American Association for Cancer Research. Ieleweke kuwa, madhara haya si ya muda bali ya kudumu ambayo yanaweza kusababisha kifo kwa mtoto, malezi na makuzi ya tabu na hata hisia mbalimbali katika maisha.

Kama wewe ni mjamzito, ni vizuri kuacha kunywa pombe.
Hata hivyo wanawake ambao walikuwa wanatumia pombe wakati wa ujauzito wasiwe na hofu sana na habari hii.
Kuna msemo uliozoeleka kitabibu kuwa ‘si kila mvutaji wa sigara anapata kansa ingawa ukweli ni kuwa wavutaji wapo katika hatari kubwa zaidi’.

Hali hii pia ina ukweli linapokuja suala la unywaji wa pombe wakati wa ujauzito kwamba si kila mtoto anaathiriwa na unywaji wa pombe ingawa hatari ya kuathirika ni kubwa zaidi.
Hivyo basi ni muhimu kwa mama mjamzito kufanya maamuzi sahihi ya maisha ya mtoto wakati wa ujauzito.

Comments

Popular posts from this blog

BIMA YA AFYA NA FAIDA ZAKE

BIMA YA AFYA NA FAIDA ZAKE By Dalus Bima ya afya ni nini? Bima ya afya ni mfumo wa kujiunga kwa hiari ama kwa lazima unaomhakikishia mwanachama kugharamiwa gharama zozote zinazojitokeza katika kupata huduma za kiafya zikiwemo kumwona daktari, kufanya vipimo pamoja na kupata matibabu na dawa kwa mwanachama husika. Bima ya afya ni kama mkataba unaoingiwa na anayetaka huduma pamoja na mtoa huduma kwa kupitia mifuko au taasisi inayowaunganisha mtoa huduma pamoja na mhitaji wa huduma husika. Mara nyingi Bima ya afya hujumuishwa kwenye makato anayoyatoa mwajiri kwa waajiriwa wake katika kufanya malipo. Pia zipo bima zinazowahusu watu binafsi, wazee na wasiojiweza, wajawazito na wengine wenye mahitaji maalumu bila kusahau wanafunzi kipindi cha masomo yao. Mara nyingi wanachama huchagua taasisi ama mifuko inayotoa bima hizi kulingana na aina, viwango na mipaka (coverage) ya Taasisi/Bima hizo. Ni ukweli uliowazi kuwa kila mfuko huweza kutofautiana na mingine katika huduma inazozitoa kwa...

FAIDA ZA NDIZI MWILINI

FAIDA ZA NDIZI MWILINI Ndizi mbivu ni tunda linalotumika sana kama mlo sehemu mbalimbali duniani. Ni tunda ambalo ni tamu na lenye virutubisho mbalimbali na muhimu kwa mwili. Baadhi ya faida za ndizi kiafya ni kusaidia moyo kufanya kazi vizuri, kupunguza uwezekano wa kupata saratani na pumu. Ndizi ni chanzo kizuri cha madini ya Potasiamu. VIRUTUBISHO VILIVYOMO KWENYE NDIZI Ndizi ya wastani ina uzito wa kama gramu 126O. Ina nishati kiasi cha kalori 110, gramu 30 za wanga na gramu 1 ya protini. Ndizi hazina fati, lehemu (cholesterol) au madini ya Sodiamu. Ndizi zina virutubisho  vifuatavyo; Vitamini B6 – 0.5 mg Manganizi- 0.3 mg Vitamini C – 9 mg Potasiamu – 450 mg Kambakamba- 3g Protini – 1 g Magneziamu – 34 mg Madini ya Foliki- 25.0 mcg Riboflavin – 0.1 mg Niacin – 0.8 mg Vitamini A – 81 IU Madini ya chuma – 0.3 mg FAIDA ZA NDIZI KIAFYA Kushusha Shinikizo la Damu Ndizi zina madini ya Potasiamu kwa wingi amb...

MTOTO KATIKA UKUAJI

HATUA MUHIMU ZA UKUAJI WA MTOTO KISAIKOLOJIA Dr. DALUS Mtoto anapitia mabadiliko mbali mbali ya kimwili,kiakili na kisaikolojia pindi anapokua anakuwa hadi kuwa mtu mzima. leo nitakuelezea hatua za ukuaji wa mtoto kisaikolojia muhimu sana katika malezi yake. hatua hizo ni kama ifatavyo 1.ORAL STAGE Mtoto anakua katika stage hii anapokuwa na umri wa,mwezi mmoja hadi mwaka mmoja.   Sasa kwa kipindi hiki erogenous zone ya mtoto inakua mdomoni, raha ya mtoto inakua kitu chochote kinachoingia mdomoni ndo maaana kipindi hiki mtoto kila kitu anachoshika anapeleka mdomoni . Hiki ndo kipindi cha kujenga strong bond kwa mtoto na mama pale mtoto anapokuwa ananyonya inamjenga kumthamini mama kuliko mtu yyte Kipindi hiki inabdi kuwa makini na vitu kama shanga,sarafu nk ambavyo akiweka mdomoni vnaweza kumkaba Hapa kama mzazi ana tabia ya kula kucha ndo kipindi mtoto nae anajifunza na kua hvo anapokua 2.ANAL STAGE Stage hii inaanza umri wa mwaka 1 hadi miaka mi 3 Hapa mtoto raha yake ni ...