Kichefuchefu na Kutapika sana wakati wa ujauzito
Dr. DALUS
Ni hali kali na inayoweza kutokea kwa mama mjamzito inayoambatana na kichefuchefu na kutapika sana au kwa namna nyingine ni kitendo endelevu cha kutapika wakati wa ujauzito kunakosababisha kupoteza uzito zaidi ya asilimia 5 ya uzito wa awali.
Huweza kupelekea kupoteza uzito, kuwa na lishe duni na kuharibika kwa usawia wa giligili, na kuharibika usawa wa kemikali mbalimbali mwilini.
Tatizo hili huambatana na kiwango kikubwa cha homoni ya HCG ambayo hutolewa kwenye kifuko cha mimba. Ukubwa wa tatizo Hutokea sana kwenye wiki 8 hadi 12 za ujauzito, na dalili hupotea wiki ya ishirini kwa wengi lakini asilimia 10 ya wenye tatizo hili.
Asilimia 0.3 hadi 2 ya wanawake wanaopata mimba katika mwaka huathiriwa na tatizo hili.
Vihatarishi Kuwa na ndugu mwenye tatizo hili kama dada, binti wa mama mwenye tatizo hili huwa kwenye hatari ya kupata tatizo hili.
Historia ya tatizo kwenye ujauzito uliopita Mimba mapacha Kuwa na hali ya kijeni inayoitwa triploidy na trisomy Kuwa na ujauzito unaoitwa molar au kuwa na historia kwenye ujauzito uliopita Wanawake wenye historia hizi pia huweza kupata tatizo hili.
Homa ya miendo Kipanda uso .
Magonjwa ya kiakili Kisukari wakati wa ujauzito .
Kiwango cha juu cha homoni ya thyroid Upungufu wa vitamin B .
Dalili Kupoteza uzito zaidi ya asilimia 5 kwenye ujauzito .
Kukaukiwa maji mwilini,
kunakosababisha kuongezeka kwa kiwango cha ketoni na kupata choo kigumu Lishe duni.
Kubadilika kwa ladha ya chakula Kuongezeka mara dufu hisia ya ubongo dhidi ya miendo .
Kubadilika kwa homoni kwa haraka wakati wa ujauzito .
Vitu vilivyomo kwenye tumbo kurudi juu ya kinywa .
Msongo wa kimwili na hali Kuvia damu kwenye macho .
Kushindwa kufanya kazi za kila siku Kuweweseka/ndoto za mchana .
Matibabu .
Nia ya matibabu ni kutibu dalili na kuwa makini kwenye kiwango cha maji kwenye damu.
Kula chakula mara kwa mara kwa kiasi kidogo na kujizuia na vyakula vinavyosababisha kichefuchefu na kutapika huwa ni jambo la muhimu.
Chai ya tangawizi imekuwa ikitumiwa zamani na hutoa uahueni sana.
Matumizi ya vitamin B6 huwa ya msingi pia kwa utibu dalili hizi kuna matibabu mengine ya kusisimua mishipa ya fahamu kupitia ngozi yanayoweza kufanyika kwenye baadhi ya hospitali hapa duniani.
Dawa za kuzuia kichefuchefu na kutapika hushauriwa kutumiaka endapo hakuna njia nyingine baada ya kupata giligili-maji ya kutosha kupitia mishipa.
Dawa kama metroclopramide, phenothiazine na ondansetron ni dawa nzuri na huwa salama kipindi cha ujauzito.
Dawa za steroid za mishipa hutumika kwa wagonjwa ambao wameshindwa kusaidiwa na dawa za kuzuia kutapika.
Mwisho kuwekewa chakula kwa njia ya mishipa hutumika kwa wagonjwa ambaowanashindwa kuwa na uzito unaotakiwa kwa sababu ya kutapika sana japokuwa naapata matibabu.
Comments