Skip to main content

FAIDA ZA NDIZI MWILINI

FAIDA ZA NDIZI MWILINI

Ndizi mbivu ni tunda linalotumika sana kama mlo sehemu mbalimbali duniani.
Ni tunda ambalo ni tamu na lenye virutubisho mbalimbali na muhimu kwa mwili.

Baadhi ya faida za ndizi kiafya ni kusaidia moyo kufanya kazi vizuri, kupunguza uwezekano wa kupata saratani na pumu. Ndizi ni chanzo kizuri cha madini ya Potasiamu.

VIRUTUBISHO VILIVYOMO KWENYE NDIZI
Ndizi ya wastani ina uzito wa kama gramu 126O.
Ina nishati kiasi cha kalori 110, gramu 30 za wanga na gramu 1 ya protini.
Ndizi hazina fati, lehemu (cholesterol) au madini ya Sodiamu.

Ndizi zina virutubisho  vifuatavyo; Vitamini B6 – 0.5 mg
Manganizi- 0.3 mg
Vitamini C – 9 mg
Potasiamu – 450 mg
Kambakamba- 3g
Protini – 1 g
Magneziamu – 34 mg
Madini ya Foliki- 25.0 mcg
Riboflavin – 0.1 mg
Niacin – 0.8 mg
Vitamini A – 81 IU
Madini ya chuma – 0.3 mg

FAIDA ZA NDIZI KIAFYA
Kushusha Shinikizo la Damu
Ndizi zina madini ya Potasiamu kwa wingi ambayo husaidia kulegeza mishipa ya damu na hivyo kupunguza shinikizo la damu au presha (blood pressure).
Pia ulaji wa madini ya potasiamu kwa wingi hupunguza hatari ya kufa kutokana na magonjwa mbalimbali.

Kupunguza Uwezekano wa Kupata Pumu (Asthma)
Ndizi zinadhaniwa kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa pumu kwa watoto. Ulaji wa ndizi moja kila siku kwa mtoto unaweza kupunguza hatari ya pumu.

Kupunguza Hatari ya Kupata Saratani Ndizi ni chanzo kizuri cha vitamini C ambayo husaidia kuondoa sumu kwenye mwili ambazo husababisha saratani kutokea.

Pia kambakamba (fibers) zinazopatikana kwenye ndizi kwa wingi husaidia kuondoa sumu kwenye utumbo zinazoweza kuchangia saratani ya utumbo. Ufanyaji Kazi wa Moyo Madini ya Potasiamu, vitamini C na B ambayo hupatikana kwa wingi kwenye ndizi huwezesha moyo kufanya kazi vizuri.

Ulaji wa vyakula vyenye Potasiamu kwa wingi na Sodiamu kidogo kama ndizi hupunguza hatari ya magonjwa kama shambulio la moyo, kiharusi na shinikizo la damu la kupanda.

Kutibu Kuharisha Kuharisha hupoteza madini mengi hasa ya Potasiamu. Ulaji wa ndizi utakusaidia kurudisha madini haya mwilini mwako.

Kuimarisha Kumbukumbui 
Ndizi zina tryptophan, aina ya protini ambayo huusika kwenye ufanyaji kazi wa kumbukumbu. Ulaji wa ndizi kwa windi inaweza kukusaidia kuongeza uwezo wako wa kufikiri.  

TAHADHARI YA MATUMIZI YA NDIZI Matumizi ya ndizi huweza kuleta madhara kwa watu wenye matatizo hasa ya figo au wanaotumia dawa kama beta blockers kama labetalol.

Ndizi zina madini mengi ya Potasiamu, hivyo kwa watu wenye matatizo ya figo hushindwa kutoa Potasiamu na kusababisha madini haya kujaa kwenye damu ambayo itaathiri afya ya mgonjwa.

Comments

Popular posts from this blog

BIMA YA AFYA NA FAIDA ZAKE

BIMA YA AFYA NA FAIDA ZAKE By Dalus Bima ya afya ni nini? Bima ya afya ni mfumo wa kujiunga kwa hiari ama kwa lazima unaomhakikishia mwanachama kugharamiwa gharama zozote zinazojitokeza katika kupata huduma za kiafya zikiwemo kumwona daktari, kufanya vipimo pamoja na kupata matibabu na dawa kwa mwanachama husika. Bima ya afya ni kama mkataba unaoingiwa na anayetaka huduma pamoja na mtoa huduma kwa kupitia mifuko au taasisi inayowaunganisha mtoa huduma pamoja na mhitaji wa huduma husika. Mara nyingi Bima ya afya hujumuishwa kwenye makato anayoyatoa mwajiri kwa waajiriwa wake katika kufanya malipo. Pia zipo bima zinazowahusu watu binafsi, wazee na wasiojiweza, wajawazito na wengine wenye mahitaji maalumu bila kusahau wanafunzi kipindi cha masomo yao. Mara nyingi wanachama huchagua taasisi ama mifuko inayotoa bima hizi kulingana na aina, viwango na mipaka (coverage) ya Taasisi/Bima hizo. Ni ukweli uliowazi kuwa kila mfuko huweza kutofautiana na mingine katika huduma inazozitoa kwa...

MTOTO KATIKA UKUAJI

HATUA MUHIMU ZA UKUAJI WA MTOTO KISAIKOLOJIA Dr. DALUS Mtoto anapitia mabadiliko mbali mbali ya kimwili,kiakili na kisaikolojia pindi anapokua anakuwa hadi kuwa mtu mzima. leo nitakuelezea hatua za ukuaji wa mtoto kisaikolojia muhimu sana katika malezi yake. hatua hizo ni kama ifatavyo 1.ORAL STAGE Mtoto anakua katika stage hii anapokuwa na umri wa,mwezi mmoja hadi mwaka mmoja.   Sasa kwa kipindi hiki erogenous zone ya mtoto inakua mdomoni, raha ya mtoto inakua kitu chochote kinachoingia mdomoni ndo maaana kipindi hiki mtoto kila kitu anachoshika anapeleka mdomoni . Hiki ndo kipindi cha kujenga strong bond kwa mtoto na mama pale mtoto anapokuwa ananyonya inamjenga kumthamini mama kuliko mtu yyte Kipindi hiki inabdi kuwa makini na vitu kama shanga,sarafu nk ambavyo akiweka mdomoni vnaweza kumkaba Hapa kama mzazi ana tabia ya kula kucha ndo kipindi mtoto nae anajifunza na kua hvo anapokua 2.ANAL STAGE Stage hii inaanza umri wa mwaka 1 hadi miaka mi 3 Hapa mtoto raha yake ni ...