Skip to main content

MIWASHO UKENI ( VAGINAL ITCHING)

MIWASHO UKENI (VAGINAL ITCHING)
By Dalus

Miwasho/michomo sehemu za siri/Ukeni huweza kusababisha  kujisikia vibaya na hasa mwanamke akiwa sehemu za watu kwa sababu hushindwa hata kujizuia kujikuna.

Miwasho ukeni huashiria kuna maambukizi au kitu fulani kigeni kimeingia sehemu hizo na hivo lengo la kipengele hiki ni kuzungumzia vitu na maambukizi yanayosababisha miwasho ukeni Nini husababisha miwasho Ukeni?

Maambukizi mbalimbali yanaweza kusababisha miwasho ukeni kama;
maambukizi ya bakiteria maambukizi ya bakiteria maeneo haya huweza kusababisha miwasho pamoja na kuhisi kama unaungua , kutoa harufu mbaya kama samaki aliyeoza na kutoa uchafu ukeni .

Magonjwa ya zinaa/sexual transmitted disease (STD) Kisonono, kaswende, trichomoniasis, virusi vya herpes na maoteo sehemu za siri inayosababishwa na  ya virusi vya human papilloma(genital warts) .

Mambukizi ya fungusi ukeni(yeast infection)- wanawake wa3 kati ya 4 watapata maambukizi haya maishani mwao.
Maambukizi haya hutokea pale ambapo wadudu hawa wamekua vihatarishi ni Kufanya mapenzi na mtu mwenye fungasi ,Ujauzito ,Kinga ya mwili kuwa chini Wanawake wote wapo hatarini kupata maambukizi haya kama kinga zao za mwili zipo chini, mbali na kuwasha mgonjwa hutoa majimaji meupe au kama maziwa ukeni .

Kukoma kwa siku za mwanamke(menopause)- kutokana na mabadiliko katika mfumo wa vichochezi mwili, wanawake waliokoma kuona siku zao mara nyingi kichochezi cha estrogeni huwa chini sana na kusababisha uke kuwa mkavu na kuta kuwa nyembamba na hivo huleta miwasho sehemu hizi- pia kwa baadhi ya wanawake wanapokuwa wananyonyesha tatizo hili linaweza kutokea pia kwa sababu hizi .

Kemikali mbalimbali zilizo kwenye sabuni, mafuta ya cream au mafuta mengine , baadhi ya pedi, karatasi za kujifutia unapotoka chooni. Yapo matibabu  ya miwasho ukeni?

Matibabu ya miwasho ukeni yapo ila hutegemea sababu ni nini, ikiwa umetumia dawa flani au mafuta yanayosababisha miwasho basi ni vema kuiacha, miwasho na miunguzo itaisha yenyewe baada ya siku chache.

Ikiwa miwasho na michomo inaendelea au uchafu unatoka ukeni basi ni vema kuonana na dakitari ili ufanyiwe uchunguzi wa sehemu hizi na upatae matibabu sahihi.

Comments

Popular posts from this blog

MTOTO KATIKA UKUAJI

HATUA MUHIMU ZA UKUAJI WA MTOTO KISAIKOLOJIA Dr. DALUS Mtoto anapitia mabadiliko mbali mbali ya kimwili,kiakili na kisaikolojia pindi anapokua anakuwa hadi kuwa mtu mzima. leo nitakuelezea hatua za ukuaji wa mtoto kisaikolojia muhimu sana katika malezi yake. hatua hizo ni kama ifatavyo 1.ORAL STAGE Mtoto anakua katika stage hii anapokuwa na umri wa,mwezi mmoja hadi mwaka mmoja.   Sasa kwa kipindi hiki erogenous zone ya mtoto inakua mdomoni, raha ya mtoto inakua kitu chochote kinachoingia mdomoni ndo maaana kipindi hiki mtoto kila kitu anachoshika anapeleka mdomoni . Hiki ndo kipindi cha kujenga strong bond kwa mtoto na mama pale mtoto anapokuwa ananyonya inamjenga kumthamini mama kuliko mtu yyte Kipindi hiki inabdi kuwa makini na vitu kama shanga,sarafu nk ambavyo akiweka mdomoni vnaweza kumkaba Hapa kama mzazi ana tabia ya kula kucha ndo kipindi mtoto nae anajifunza na kua hvo anapokua 2.ANAL STAGE Stage hii inaanza umri wa mwaka 1 hadi miaka mi 3 Hapa mtoto raha yake ni ...

BIMA YA AFYA NA FAIDA ZAKE

BIMA YA AFYA NA FAIDA ZAKE By Dalus Bima ya afya ni nini? Bima ya afya ni mfumo wa kujiunga kwa hiari ama kwa lazima unaomhakikishia mwanachama kugharamiwa gharama zozote zinazojitokeza katika kupata huduma za kiafya zikiwemo kumwona daktari, kufanya vipimo pamoja na kupata matibabu na dawa kwa mwanachama husika. Bima ya afya ni kama mkataba unaoingiwa na anayetaka huduma pamoja na mtoa huduma kwa kupitia mifuko au taasisi inayowaunganisha mtoa huduma pamoja na mhitaji wa huduma husika. Mara nyingi Bima ya afya hujumuishwa kwenye makato anayoyatoa mwajiri kwa waajiriwa wake katika kufanya malipo. Pia zipo bima zinazowahusu watu binafsi, wazee na wasiojiweza, wajawazito na wengine wenye mahitaji maalumu bila kusahau wanafunzi kipindi cha masomo yao. Mara nyingi wanachama huchagua taasisi ama mifuko inayotoa bima hizi kulingana na aina, viwango na mipaka (coverage) ya Taasisi/Bima hizo. Ni ukweli uliowazi kuwa kila mfuko huweza kutofautiana na mingine katika huduma inazozitoa kwa...

FAIDA ZA NDIZI MWILINI

FAIDA ZA NDIZI MWILINI Ndizi mbivu ni tunda linalotumika sana kama mlo sehemu mbalimbali duniani. Ni tunda ambalo ni tamu na lenye virutubisho mbalimbali na muhimu kwa mwili. Baadhi ya faida za ndizi kiafya ni kusaidia moyo kufanya kazi vizuri, kupunguza uwezekano wa kupata saratani na pumu. Ndizi ni chanzo kizuri cha madini ya Potasiamu. VIRUTUBISHO VILIVYOMO KWENYE NDIZI Ndizi ya wastani ina uzito wa kama gramu 126O. Ina nishati kiasi cha kalori 110, gramu 30 za wanga na gramu 1 ya protini. Ndizi hazina fati, lehemu (cholesterol) au madini ya Sodiamu. Ndizi zina virutubisho  vifuatavyo; Vitamini B6 – 0.5 mg Manganizi- 0.3 mg Vitamini C – 9 mg Potasiamu – 450 mg Kambakamba- 3g Protini – 1 g Magneziamu – 34 mg Madini ya Foliki- 25.0 mcg Riboflavin – 0.1 mg Niacin – 0.8 mg Vitamini A – 81 IU Madini ya chuma – 0.3 mg FAIDA ZA NDIZI KIAFYA Kushusha Shinikizo la Damu Ndizi zina madini ya Potasiamu kwa wingi amb...