Skip to main content

Posts

FISTULA

FAHAMU ZAIDI KUHUSU FISTULA By Dr. DALUS Kwa kitaalamu fistula hujulikana kama njia isiyo ya kawaida inayounganisha mfuko wa mkojo na uke, ambayo huruhusu mkojo na/au haja kubwa kutoka  bila kujizuia kwenye kuta za uke. Nini hutokea? Tatizo la kushindwa kujizuia kujikojolea na/au kupitisha haja kubwa kwenye tupu ya mwanamke linalojulikana kama fistula hutokea baada ya mwanamke kupata madhara kipindi cha kujifungua kutokana na kuwa kwenye uchungu wa kujifungua kwa muda mrefu (Prolonged and obstructed labor), kutokana na kichwa cha mtoto kushindwa kupita kwa urahisi kwenye tupu ya  mwanamke. Hali hii husababisha tishu za kwenye tupu ya mwanamke, kibofu cha mkojo na puru (rectum), kugandamizwa kati ya kichwa cha mtoto na nyonga za mwanamke. Hii husababisha mfumo wa damu kwenye tishu hizi kuharibika na tishu kukosa damu na kuwa katika hali inayojulikana kitaalamu kama ischemic necrosis. Baadaye tundu hutokea kati ya tupu ya mwanamke na kibofu cha mkojo au kati ya tupu ya mwa...

DALILI ZA UJAUZITO

DALILI ZA UJAUZITO By Dr.  DALUS Dalili za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke mmoja  na mwanamke mwingine, ingawa kuchelewa au kukosa hedhi ni dalili moja muhimu sana ya ujauzito. Ni muhimu kuzitambua na kuzifahamu dalili hizi kwa sababu zinaweza kusaidia kujua kama kweli umeshika ujauzito au la  pamoja na kuweza kutofautisha matatizo mengine yanayoshahabiana kwa dalili na  ujauzito. Hebu sasa tuangalie dalili na ishara za ujauzito: Kutokwa damu kidogo ukeni wakati kiumbe kikipandikizwa kwenye mfuko wa uzazi, ingawa siyo wanawake wote hupatwa na dalili hii. Kukosa hedhi, hii ni moja ya dalili kubwa ya ujauzito . Maumivu kwenye matiti na kuvimba matiti (huweza kutokea kati ya wiki ya 1 hadi ya 2) Uchovu, wanawake wengi huhisi uchovu na  na hali ya kutopenda kufanya lolote. Kupoteza ladha au kuhisi ladha ya chuma mdomoni Kuongezeka kwa hisia ya harufu, kipindi cha ujauzito wanawake wengi huongezeka hisia ya harufu Kic...

BISHOP SCORE

Understanding Your Bishop Score and What to Expect from Labor Induction Medical. Written by Dr. DALUS The Bishop score Is a system used by medical professionals to decide how likely it is that you will go into labor soon. They use it to determine whether they should recommend induction, and how likely it is that an induction will result in a vaginal birth. The score considers different factors about your cervix and the position of your baby. Each factor is given a grade, and then these grades are added up to give you an overall score. It’s called the Bishop score because it was developed by Dr. Edward Bishop in the 1960s. SCORE Understanding your score There are several factors that your doctor will consider when calculating your score: Dilation of the cervix. This means how far your cervix has opened in centimeters. Effacement of the cervix. This means how thin your cervix is. It is normally about 3 centimeters long. It gradually becomes thinner as labor progresses. C...

KUHARIBIKA KWA MIMBA (Abortion)

KUHARIBIKA KWA MIMBA (Abortion) By Dr. DALUS Tatizo la mimba kutoka au kutolewa ni jambo ambalo limewakumba kina mama wengi walio katika umri wa kuzaa. Aidha mijadala kuhusu kuhalalishwa au kuendelea kuharamishwa kwa utoaji mimba ni jambo linalochukua nafasi ya mazungumzo ya kila siku katika maisha yetu. Kwa baadhi ya nchi, suala la utoaji mimba ni jambo lililohalalishwa kisheria ingawa kwa nchi kama Tanzania, suala hili halijahalalishwa isipokuwa tu pale panapokuwa na sababu za kitabibu zinazolazimisha kufanya hivyo. Nini maana ya mimba kutoka? Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), utokaji mimba (abortion) hutokea pale ambapo kiumbe (mimba) kilicho chini ya wiki 22 kinapotoka kwa sababu moja ama nyingine, au kinapotolewa kwa njia yeyote ile. Aidha shirika la Afya limekwenda mbali zaidi na kutoa maana nyingine ya utokaji mimba kuwa ni pale mtoto (kiumbe) anapozaliwa akiwa na uzito wa chini ya gram 500. Aidha baadhi ya matabibu hupendelea kutumia neno 'abortion' ...

MADHARA YA UNYWAJI YA POMBE WAKATI WA UJAUZITO

Madhara ya Unywaji wa Pombe wakati wa Ujauzito. By Dr. DALUS Kati ya mambo ambayo watu wengi hawatilii maanani sana ni unywaji wa pombe wakati wa ujauzito. Nimekuwa nikiwaona akina mama wajawazito wengi wakinywa pombe kwenye sehemu za starehe na sherehe mbalimbali. Hata hivyo si nia ya makala hii kuwazuia kunywa pombe bali kuwapa elimu sahihi juu ya unywaji wa pombe wakati wa ujauzito. Baadhi ya wataalam wanasema unywaji wa wastani wakati wa ujauzito ni kitu ambacho kinaweza kukubalika ingawa wapo baadhi ya wataalamu wengine wanaoamini kuwa unywaji wa hata glasi moja ya mvinyo (wine) kwa wiki huhatarisha afya ya mtoto wako. Hata hivyo haijulikani kwa hakika, ni kiasi gani cha pombe ni salama kwa makuzi sahihi ya mtoto wako tumboni. Wataalamu wengi wanashauri kuacha pombe kabisa wakati wa ujauzito. Pombe inaweza kuleta madhara makubwa kwa mtoto wako bila wewe kuhisi madhara yake. Na yanaweza kuwa madhara ya kudumu ambayo ataishi nayo maisha yake yote. Aidha kuna dhana imejengek...

KIFAFA CHA MIMBA (ECLAMPSIA)

TATIZO LA KIFAFA CHA MIMBA (ECLAMPSIA) By Dr. DALUS Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito). Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito. Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni. Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto wali...

KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA WAKATI WA UJAUZITO

Kichefuchefu na Kutapika sana wakati wa ujauzito Dr. DALUS Ni hali kali na inayoweza kutokea kwa mama mjamzito inayoambatana na kichefuchefu na kutapika sana au kwa namna nyingine ni kitendo endelevu cha kutapika wakati wa ujauzito kunakosababisha kupoteza uzito zaidi ya asilimia 5 ya uzito wa awali. Huweza kupelekea kupoteza uzito, kuwa na lishe duni na kuharibika kwa usawia wa giligili, na kuharibika usawa wa kemikali mbalimbali mwilini. Tatizo hili huambatana na kiwango kikubwa cha homoni ya HCG ambayo hutolewa kwenye kifuko cha mimba. Ukubwa wa tatizo Hutokea sana kwenye wiki 8 hadi 12 za ujauzito, na dalili hupotea wiki ya ishirini kwa wengi lakini asilimia 10 ya wenye tatizo hili. Asilimia 0.3 hadi 2 ya wanawake wanaopata mimba katika mwaka huathiriwa na tatizo hili. Vihatarishi Kuwa na ndugu mwenye tatizo hili kama dada, binti wa mama mwenye tatizo hili huwa kwenye hatari ya kupata tatizo hili. Historia ya tatizo kwenye ujauzito uliopita Mimba mapacha Kuwa na hali ya kij...