Zijue faida za kula tende kiafya Tende ni matunda maarufu sana kutokana na faida kedekede zipatikanazo. Kwa kingereza huitwa dates, kwa kihindi huitwa khajur, kwa lugha ya kitaalamu (botanical name)huitwa Phoenix dactiylifera. Tende zimetunukiwa viambata muhimu mno kama protini, wanga, vitamins B1, B3,B5,A1,pia madini kama kalsiam, magniziam, manganizi, na kopa. Tende zinaweza kuchanganywa na maziwa ili kuongeza ufanisi, au kuchanganya na asali, unaweza kufanya juisi ya tende maridhawa, au kula hivi hivi. Miongoni mwa faida zinazopatikana kwa kutumia juisi ya tende au tende zenyewe ni kama ifuatavyo; Kuimarisha mifupa (bones),misuli na meno, tende husaidia sana kuimarisha afya ya mifupa, misuli na meno ya mlaji. Sababu tende zina manganese kwa wingi, kalsiam, selenium, pamoja na copper. Husaidia kuimarisha afya ya macho (eye sight), ulaji wa tende au juisi yake maridhawa. Kutokana na upatikanaji wa vitamini kwa wingi. Husaidia kwa wenye saratani. Kama ambavyo tafiti iliyofa...