FAHAMU ZAIDI KUHUSU FISTULA By Dr. DALUS Kwa kitaalamu fistula hujulikana kama njia isiyo ya kawaida inayounganisha mfuko wa mkojo na uke, ambayo huruhusu mkojo na/au haja kubwa kutoka bila kujizuia kwenye kuta za uke. Nini hutokea? Tatizo la kushindwa kujizuia kujikojolea na/au kupitisha haja kubwa kwenye tupu ya mwanamke linalojulikana kama fistula hutokea baada ya mwanamke kupata madhara kipindi cha kujifungua kutokana na kuwa kwenye uchungu wa kujifungua kwa muda mrefu (Prolonged and obstructed labor), kutokana na kichwa cha mtoto kushindwa kupita kwa urahisi kwenye tupu ya mwanamke. Hali hii husababisha tishu za kwenye tupu ya mwanamke, kibofu cha mkojo na puru (rectum), kugandamizwa kati ya kichwa cha mtoto na nyonga za mwanamke. Hii husababisha mfumo wa damu kwenye tishu hizi kuharibika na tishu kukosa damu na kuwa katika hali inayojulikana kitaalamu kama ischemic necrosis. Baadaye tundu hutokea kati ya tupu ya mwanamke na kibofu cha mkojo au kati ya tupu ya mwa...
Good Health For All